factograf
SW

Omikron

Omikron

Omikron, yaani "o ndogo" (Ο ο) ni herufi ya 15 katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama ο (alama ya kawaida) au Ο (alama kubwa). Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu ikiwa alama ya namba 70.

Asili ya omikron ni herufi ya Kifinisia "ayin" . Herufi zilizotokana nayo katika alfabeti zilizofuata Kigiriki ni O katika alfabeti ya Kilatini na katika alfabeti ya Kisirili vilevile.

Matamshi yake yalikuwa "o".

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, ο inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hisabati na fizikia.

Read next

In 90 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article