factograf
SW

Tau

Tau

Tau (Τ τ) ni herufi ya 19 katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama τ (alama ya kawaida) au Τ (alama kubwa). Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu ikiwa alama ya namba 300.

Asili ya tau ni herufi ya Kifinisia "taw" (𐤕). Herufi zilizotokana nayo katika alfabeti zilizofuata Kigiriki ni T katika alfabeti ya Kilatini na Te (Т, т) katika alfabeti ya Kisirili.

Matamshi yake ilikuwa "t".

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, τ inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hisabati na fizikia.

Read next

In 89 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article