factograf
SW

Bamako

Bamako

Key facts

idadi ya watu4,227,569
ni mfano wajiji, Mgawanyiko wa kiutawala wa ngazi ya kwanza
NchiMali
mkuu wa serikaliAdama Sangaré
All data from the card 2
Nchi
Mali
Mkoa
Bamako Capital District
Bamako nchini Mali
Bamako nchini Mali
Bamako kutoka mlimani
Bamako kutoka mlimani
Watu huchunguza takataka shambani Bamako
Watu huchunguza takataka shambani Bamako
Matatu au daladala za Bamako huitwa "sotruma".
Matatu au daladala za Bamako huitwa "sotruma".
4 images

Bamako ni mji mkuu wa Mali pamoja na kuwa mji mkubwa nchini ikiwa na wakazi 4,227,569 mwaka 2022. Uko mwambaoni mwa mto Niger kusini mwa nchi.

Historia

Bamako ilianzishwa kama mji katika karne ya 17 BK na machifu wa kabila la Niare Seribadian Niaré na Soumba Coulibaly. Jina la asili lilikuwa "Bammako" (Kibambara: "bwawa la mamba"). Bamako ilikuwa soko muhimu pamoja na mji wa elimu ya Kiislamu katika Dola la Mali. Wakati wa karne ya 19 sifa zake zilikuwa zimepungua. Mwaka 1883 Wafaransa walikuta kijiji kikubwa cha watu 600 chenye kuta za ulinzi.

Wakati wa ukoloni Bamako ikawa makao makuu ya koloni la Senegal ya Juu-Niger mwaka 1899 halafu mji mkuu wa Sudan ya Kifaransa mwaka 1920. Ikulu ya Koulouba ilijengwa 1907 kama makao makuu ya gavana ikawa ikulu ya rais baada ya uhuru.

Mwaka 1904 Bamako iliunganishwa na reli ya Dakar - Niger. Majengo mengine ya siku zile yalikuwa kanisa kuu la katoliki mwaka 1927, daraja la kwanza juu ya mto Niger 1947 na misikiti mkuu mwaka 1948.

Mwaka 1955 Bamako ilipewa cheo cha mji kufuatana na sheria ya kifaransa. Meya mwafrika wa kwanza alikuwa Modibo Keïta mwaka 1956.

Tarehe 22 Septemba 1960 Mali ikapata uhuru wake Bamako ikawa mji mkuu wa jamhuri.

Majengo

Majengo mazuri mjini ni maktaba ya kitaifa, mnara ya Tour BCEAO, msikiti kuu na daraja la mfalme Fahd (Pont du Roi Fahd). Hata makumbusho ya kitaifa, makumbusho ya Muso Kunda, makumbusho ya mkoa wa Bamako, zoo ya Bamako na kilima cha "Point G" chenye uchoraji wa mwambani zinapendeza vilevile.

Kuna uwanja wa ndege cha kimataifa na reli ya kwenda Koulikoro katika mashariki ya Mali na Dakar (Senegal).

Viungo vya Nje

  • Bamako-culture.org (Kifaransa) Ilihifadhiwa 21 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.
  • Bamako at Cités du Monde (Kifaransa) Ilihifadhiwa 4 Februari 2005 kwenye Wayback Machine.
  • The Bamako Appeal Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
  • Makala kuhusu muziki wa Mali toka New York Times
  • Makala zinazohusu muziki toka New York Times

Read next

In 161 languages

swAfrikaansአማርኛaragonésالعربيةܐܪܡܝܐمصرىasturianuKotavaazərbaycancaتۆرکجهбашҡортсаBasa Baliбеларуская (тарашкевіца)беларускаябългарскиbamanankanবাংলাབོད་ཡིགbrezhonegbosanskicatalà閩東語 / Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄нохчийнCebuanoکوردیčeštinaчӑвашлаCymraegdanskDeutschZazakiΕλληνικάEnglishEsperantoespañoleestieuskaraestremeñuفارسیFulfuldesuomivõrofrançaisNordfriiskFryskGaeilgeGàidhliggalegoAvañe'ẽHausa客家語 / Hak-kâ-ngîעבריתहिन्दीFiji HindihrvatskihornjoserbsceKreyòl ayisyenmagyarհայերենinterlinguaBahasa IndonesiaInterlingueIlokanoIdoíslenskaitaliano日本語JawaქართულიTaqbaylitJjuKabɩyɛKongoKumoringқазақша한국어kurdîкыргызчаLatinaLëtzebuergeschLingua Franca NovaLigurelombardlietuviųlatviešuмокшеньMalagasyMāoriMinangkabauмакедонскиമലയാളംमराठीкырык марыBahasa MelayuمازِرونیNapulitanoPlattdüütschNederlandsnorsk nynorsknorskNovialߒߞߏDiné bizaadChi-ChewaoccitanlivvinkarjalaиронਪੰਜਾਬੀPapiamentupolskiPiemontèisپنجابیپښتوportuguêsromânăрусскийрусиньскыйIkinyarwandaᱥᱟᱱᱛᱟᱲᱤsardusicilianuScotsسنڌيdavvisámegiellasrpskohrvatski / српскохрватскиසිංහලSimple EnglishslovenčinaslovenščinaanarâškielâchiShonaSoomaaligashqipсрпски / srpskiSiSwatisvenskaślůnskiதமிழ்తెలుగుтоҷикӣไทยTagalogTürkçeудмуртукраїнськаاردوoʻzbekcha / ўзбекчаvènetovepsän kel’Tiếng ViệtVolapükWinaray吴语მარგალურიייִדישYorùbáZeêuws閩南語 / Bân-lâm-gí粵語中文

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article