factograf
SW

Polynesia ya Kifaransa

Polynesia ya Kifaransa

Key facts

idadi ya watu278,786
kuanzishwa1842
NchiUfaransa
mji mkuuPapeete
BaraAustralia na Pasifiki
ipo katika eneo la kiutawalaEneo la ng'ambo la Ufaransa


Polinesia ya Kifaransa (kwa Kifaransa: Polynésie française; kwa Kitahiti: Pōrīnetia Farāni) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa katika Pasifiki ya kusini. Eneo lake ni mafunguvisiwa mbalimbali ya Polinesia.

Kisiwa kinachojulikana zaidi ni Tahiti pamoja na mji mkuu wake wa Papeete ambayo ni pia mji mkuu wa eneo lote.

Jiografia

Ramani ya Polinesia ya Kifaransa
Ramani ya Polinesia ya Kifaransa

Visiwa, funguvisiwa na atolli za Polinesia ya Kifaransa kwa jumla vina eneo la nchi kavu la km² 4,167 jumla vilivyosambazwa katika kilomita za mraba 2,500,000 za bahari.

Visiwa vyote vimegawiwa katika tarafa tano ambazo ni vikundi vya visiwa vyenye mafunguvisiwa ndani yake; ni kama zifuatazo:

  • Visiwa vya Marquesas katika kaskazini, karibu zaidi na Hawaii, penye makundi mbili ya visiwa, vya kaskazini na ya kusini
  • Visiwa vya Tuamoto-Gambier ni eneo kubwa la Polynesia ya Kifaransa lenye mafunguvisiwa mawili: Tuamoto (atolli 76) na Gambier (visiwa 26)
  • Visiwa vya Shirika (Visiwa vya Society) 13 vyenye asili ya kivolkeno ambavyo ni sehemu yenye wakazi wengi; vimegawiwa katika tarafa mbili za:
    • tarafa ya Visiwa upande wa upepo pamoja na kisiwa kikuu cha Tahiti chenye nusu ya wakazi wote wa Polynesia ya Kifaransa
    • tarafa ya Visiwa mbali na upepo
  • Visiwa vya Austral (Visiwa vya Kusini) vyenye mafunguvisiwa mawili: Tubuaï na Bass.

Watu

Wakazi ni 268,270 (sensa ya mwaka 2012), ambao kati yao 2/3 ni Wapolinesia asilia na 11,9% ni Wazungu.

Kati yao wote, 68,5% wanatumia kwa kawaida lugha ya Kifaransa, iliyo lugha rasmi pekee.

Upande wa dini, 54% ni Waprotestanti, 30% ni Wakatoliki, halafu kuna Wamormoni na Mashahidi wa Yehova.

Tazama pia


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Read next

In 147 languages

swAcèhAfrikaansአማርኛaragonésÆngliscअंगिकाالعربيةمصرىasturianuazərbaycancaتۆرکجهбашҡортсаBasa BaližemaitėškaBikol Centralбеларуская (тарашкевіца)беларускаябългарскиभोजपुरीবাংলাবিষ্ণুপ্রিয়া মণিপুরীbrezhonegbosanskicatalà閩東語 / Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄CebuanoTsetsêhestâheseکوردیčeštinaCymraegdanskDeutschZazakiދިވެހިބަސްΕλληνικάEnglishEsperantoespañoleestieuskaraفارسیsuomivõroføroysktfrançaisarpetanNordfriiskFryskGaeilgeGagauzkriyòl gwiyannenGàidhliggalego客家語 / Hak-kâ-ngîHawaiʻiעבריתहिन्दीFiji HindihrvatskimagyarհայերենBahasa IndonesiaIdoíslenskaitaliano日本語Jawaქართულიқазақша한국어kernowekкыргызчаLatinaLëtzebuergeschLingua Franca NovaLimburgsLigureລາວlietuviųlatviešuMalagasyMāoriмакедонскиമലയാളംмонголဘာသာမန်मराठीкырык марыBahasa MelayuمازِرونیNederlandsnorsk nynorsknorskoccitanиронਪੰਜਾਬੀKapampanganpolskiPiemontèisپنجابیپښتوportuguêsRuna SimiromânăрусскийIkinyarwandasardusicilianuScotsdavvisámegiellasrpskohrvatski / српскохрватскиတႆးසිංහලSimple EnglishslovenčinaslovenščinaGagana SamoachiShonashqipсрпски / srpskiSundasvenskaślůnskiதமிழ்తెలుగుтоҷикӣไทยTagaloglea faka-TongaTürkçeтатарча / tatarçareo tahitiئۇيغۇرچە / Uyghurcheукраїнськаاردوoʻzbekcha / ўзбекчаvènetoTiếng ViệtWinarayWolof吴语მარგალურიYorùbá閩南語 / Bân-lâm-gí粵語中文

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article