factograf
SW

Nauru

Nauru

Key facts

idadi ya watu13,650
kuanzishwa31 Januari 1968
ni mfano wanchi za visiwa, Jamhuri
NchiNauru
mji mkuuYaren
mkuu wa nchiDavid Adeang
mkuu wa serikaliDavid Adeang
BaraPasifiki na Australia
SarafuDola ya Australia
lugha rasmiKinauru


Nauru, rasmi kama Jamhuri ya Nauru, ni nchi ndogo ya kisiwa iliyoko katika eneo la Mikronesia katika Pasifiki. Iko kaskazini-mashariki mwa Australia, inayozungukwa na Bahari ya Pasifiki, na majirani yake wa karibu ni Kiribati upande wa mashariki na Visiwa vya Marshall upande wa kaskazini. Nauru ina wakazi takriban 10,000, na kwa hiyo iko kati ya nchi ndogo zaidi duniani kwa idadi ya watu. Ikiwa na eneo la kilomita za mraba 21 tu, pia ni moja ya nchi ndogo zaidi kwa eneo la ardhi. Mji mkubwa zaidi na mji mkuu wa Nauru ni Yaren, ambayo hutumika kama kitovu cha utawala wa nchi hiyo licha ya ukubwa wake mdogo.

Kisiwa jirani zaidi ni Banaba katika Kiribati chenye umbali wa km 300.

Nauru haina mji mkuu rasmi.

Historia

Nauru imekaliwa na mchanganyiko wa watu kutoka Polynesia na Mikronesia tangu karne nyingi (miaka 3,000 hivi).

Katika karne ya 19 kisiwa kilitwaliwa na Ujerumani kama sehemu ya makoloni yake ya Pasifiki.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kilikuwa eneo lindwa chini ya Umoja wa Mataifa (UM) na utawala ulikuwa mikononi mwa nchi tatu: Australia, New Zealand na Uingereza.

Uhuru ulipatikana tangu 1968.

Watu

Wakazi wengi (58%) ni wenyeji, wakifuatwa na watu kutoka visiwa vingine vya Pasifiki (26%), Wazungu (8%) na Wachina (8%).

Karibu wote (95%) ni wanene mno, hivyo hali ya afya si nzuri, hasa upande wa kisukari (40%).

Lugha

Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Nauru: Kiingereza (lugha rasmi), Kinauru (lugha ya mawasiliano), na pijini inayounganisha Kiingereza, Kichina na Kiaustronesia.

Dini

Wakazi wengi ni Wakristo (Waprotestanti na Wakatoliki kwa uwiano wa 2:1), wakifuatwa na wafuasi wa Bahai (10%) na Wabuddha (9%).

Uchumi

Uchumi wa Nauru ulitegemea fosfeti iliyopatikana kisiwani kwa wingi. Kwa miaka kadhaa kisiwa kilikuwa nchi tajiri kabisa. Hadi mwaka 2001 huduma za hospitali zilikuwa bure, hapakuwa na kodi, na watu wengi walikuwa na magari mawili au matatu.

Tangu kumalizika kwa fosfeti hali ya kiuchumi imekuwa ngumu sana. 90% za wananchi wanakosa kazi. Serikali haina pesa za kutosha tena, huduma nyingi zimekwama, hata imeanza kupokea misaada kutoka Australia.

Tazama pia


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Read next

In 224 languages

swаԥсшәаAcèhAfrikaansAlemannischአማርኛPangcaharagonésÆngliscअंगिकाالعربيةالدارجةمصرىঅসমীয়াasturianuKotavaazərbaycancaتۆرکجهбашҡортсаBasa BaližemaitėškaBikol Centralбеларуская (тарашкевіца)беларускаяBetawiбългарскиBislamaBanjarবাংলাབོད་ཡིགবিষ্ণুপ্রিয়া মণিপুরীbrezhonegbosanskiбуряадcatalàChavacano de Zamboanga閩東語 / Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄нохчийнCebuanoTsetsêhestâheseکوردیqırımtatarcačeštinaсловѣньскъ / ⰔⰎⰑⰂⰡⰐⰠⰔⰍⰟCymraegdanskdagbanliDeutschZazakidolnoserbskiडोटेलीދިވެހިބަސްཇོང་ཁΕλληνικάEnglishEsperantoespañoleestieuskaraestremeñuفارسیFulfuldesuomivõroføroysktfrançaisarpetanNordfriiskfurlanFryskGaeilgeGagauzkriyòl gwiyannenGàidhliggalegoگیلکیAvañe'ẽगोंयची कोंकणी / Gõychi KonknniBahasa Hulontalo𐌲𐌿𐍄𐌹𐍃𐌺ગુજરાતીGaelgHausa客家語 / Hak-kâ-ngîעבריתहिन्दीFiji HindihrvatskihornjoserbsceKreyòl ayisyenmagyarհայերենinterlinguaBahasa IndonesiaInterlingueIlokanoIdoíslenskaitaliano日本語PatoisJawaქართულიQaraqalpaqshaKarai-karaiKumoringқазақшаಕನ್ನಡ한국어къарачай-малкъарkurdîkernowekкыргызчаLatinaLadinoLëtzebuergeschлезгиLingua Franca NovaLimburgsLigureLadinlombardlietuviųlatviešuMalagasyMāoriMinangkabauмакедонскиമലയാളംмонголꯃꯤꯇꯩ ꯂꯣꯟमराठीкырык марыBahasa MelayuMaltiMirandésမြန်မာဘာသာمازِرونیNedersaksiesPlattdüütschनेपालीनेपाल भाषाNederlandsnorsk nynorsknorskNovialNupeoccitanlivvinkarjalaଓଡ଼ିଆиронਪੰਜਾਬੀKapampanganPapiamentupolskiPiemontèisپنجابیپښتوportuguêsRuna SimirumantschromânăarmãneashtiрусскийIkinyarwandaसंस्कृतम्саха тылаsardusicilianuScotsسنڌيdavvisámegiellasrpskohrvatski / српскохрватскиတႆးසිංහලSimple EnglishslovenčinaslovenščinaGagana SamoaanarâškielâchiShonaSoomaaligashqipсрпски / srpskiSundasvenskaślůnskiSakizayaதமிழ்TayalతెలుగుтоҷикӣไทยTagaloglea faka-Tongatoki ponaTok PisinTürkçeSeediqтатарча / tatarçaTwireo tahitiудмуртئۇيغۇرچە / Uyghurcheукраїнськаاردوoʻzbekcha / ўзбекчаvènetovepsän kel’Tiếng ViệtVolapükWinarayWolof吴语isiXhosaმარგალურიייִדישYorùbáVahcuenghZeêuws文言閩南語 / Bân-lâm-gí粵語中文

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article