
Papa Adeodato I (pia Adeodatus, Deodatus, Deusdedit) alikuwa Papa kuanzia tarehe 19 Oktoba 615 hadi kifo chake tarehe 8 Novemba 618. Alitokea Roma, Italia. Jina la baba yake lilikuwa Stephanus, ambaye alikuwa shemasi mdogo.
Alimfuata Papa Bonifasi IV akafuatwa na Papa Bonifasi V.
Kabla ya kuchaguliwa, alitoa huduma ya kipadri kwa miaka 40. Alikuwa padri wa kwanza kuchaguliwa kuwa Papa tangu Yohane II mwaka 533. Baadaye alikuza idadi ya mapadri na kuwapa nafasi zilizokuwa zimeshikwa na wamonaki kadiri ya sera ya Papa Gregori I na Papa Bonifasi IV.
Kweli alijulikana kwa kupenda wakleri na waumini wake pamoja na unyofu na hekima yake.
Matumizi ya kwanza ya mihuri ya risasi au bullae kwenye nyaraka za Kipapa yanahusishwa naye.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
- Orodha ya Mapapa
Viungo vya nje
- Kuhusu Papa Adeodato I katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Adeodato I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
