factograf
SW
Sign in

Familia ya ndege wakubwa wa bahari

Albatrosi

Albatrosi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Procellariiformes (Ndege kama walinzi)
Familia: Diomedeidae (Ndege walio na mnasaba na albatrosi)
Gray, 1840

Albatrosi Albatrosi utosi-mweupe

Albatrosi utosi-mweupe
Uainishaji wa kisayansi Ngazi za chini

Jenasi 4:

Albatrosi (kutoka Kiing.: albatross) ni ndege wakubwa wa bahari katika familia Diomedeidae. Baina ya spishi hizi yuko ndege wenye mabawa marefu kabisa kuliko ndege wote duniani. Albatrosi Mlizi ana mabawa ambayo mawili pamoja yana urefu wa sm 310 kwa wastani na urefu mkubwa kabisa uliopimwa ulikuwa sm 370. Rangi zao zinatofautiana kutoka nyeupe na mabawa kijivu hafifu hadi mwili wote kijivucheusi. Wana domo kubwa sana lenye ncha kwa umbo la kulabu. Mirija miwili ya pua inapitia pande zote mbili za domo.

Ndege hawa huenda mbali sana wakiruka angani na wanaweza kuzunguka dunia. Hawapigi mabawa sana baada ya kuruka, lakini wananyiririka kwa mabawa yaliyonyooshwa. Huwakamata ngisi, samaki na gegereka na hula mizoga pia. Kwa kawaida albatrosi huyatengeneza matago yao kwenye visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Kabla ya kujamiiana dume na jike hutenga dansi ya kanuni kaida. Jike hulitaga yai moja tu.

Spishi za Afrika

  • Diomedea amsterdamensis, Albatrosi wa Kisiwa Amsterdam (Amsterdam Albatross)
  • Diomedea dabbenena, Albatrosi wa Tristan (Tristan Albatross)
  • Diomedea epomophora, Albatrosi Mfalme (Southern Royal Albatross)
  • Diomedea exulans, Albatrosi Mlizi (Wandering Albatross)
  • Phoebetria fusca, Albatrosi Kijivucheusi (Sooty Albatros)
  • Phoebetria palpebrata, Albatrosi Mgongo-kijivu (Light-mantled Albatros)
  • Thalassarche bulleri, Albatrosi wa Buller (Buller's Albatross)
  • Thalassarche carteri, Albatrosi Domo-njano wa Bahari ya Hindi (Indian Yellow-nosed Albatross)
  • Thalassarche cauta, Albatrosi Utosi-mweupe (Shy Albatross)
  • Thalassarche chlororhynchos, Albatrosi Domo-njano wa Bahari ya Atlantiki (Atlantic Yellow-nosed Albatross)
  • Thalassarche chrysostoma, Albatrosi Kichwa-kijivu (Grey-headed Albatross)
  • Thalassarche melanophris, Albatrosi Nyusi-nyeusi (Black-browed Albatross)
  • Thalassarche salvini, Albatrosi wa Salvin (Salvin's Albatross)

Spishi za mabara mengine

  • Diomedea antipodensis (Antipodean Albatross)
  • Diomedea sanfordi (Northern Royal Albatross)
  • Phoebastria albatrus (Short-tailed Albatross)
  • Phoebastria immutabilis (Laysan Albatross)
  • Phoebastria irrorata (Waved Albatross)
  • Phoebastria nigripes (Black-footed Albatross)
  • Thalassarche eremita (Chatham Albatross)
  • Thalassarche impavida (Campbell Albatross)

Picha

Albatrosi wa Kisiwa cha Amsterdam
Albatrosi wa Kisiwa cha Amsterdam
Albatrosi wa Tristan
Albatrosi wa Tristan
Albatrosi mfalme
Albatrosi mfalme
Albatrosi mlizi
Albatrosi mlizi
Albatrosi kijivucheusi
Albatrosi kijivucheusi
Albatrosi mgongo-kijivu
Albatrosi mgongo-kijivu
Albatrosi wa Buller
Albatrosi wa Buller
Albatrosi domo-njano wa Bahari ya Hindi
Albatrosi domo-njano wa Bahari ya Hindi
Albatrosi utosi-mweupe
Albatrosi utosi-mweupe
Albatrosi domo-njano wa Bahari ya Atlantiki
Albatrosi domo-njano wa Bahari ya Atlantiki
Albatrosi kichwa-kijivu
Albatrosi kichwa-kijivu
Albatrosi nyusi-nyeusi
Albatrosi nyusi-nyeusi
12 images

Read next

In 96 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article