factograf
SW
Sign in

Rapa

Tech N9ne

Tech N9ne

Key facts

tarehe ya kuzaliwa8 Novemba 1971
kazimwimbaji, Mtunzi wa nyimbo
mahali alipozaliwaKansas City
All data from the card 6
Jina la kuzaliwa
Aaron Dontez Yates
Amezaliwa
8 Novemba 1971
Chimbuko
Kansas City, Missouri, Marekani
Aina ya muziki
Midwestern hip-hoprap rockhardcore hip hophorrorcorechopper
Miaka ya kazi
1991–sasa
Studio
Strange RBC JCOR Interscope Qwest Perspective A&M Warner Bros.

Aaron Dontez Yates (amezaliwa Novemba 8, 1971), anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Tech N9ne (inatamkwa "tech nine"), ni rapa, mwandishi wa nyimbo, na mwimbaji kutoka nchini Marekani. Mnamo mwaka 1999, yeye na mshirika wake wa kibiashara Travis O'Guin walianzisha studio ya muziki ya Strange Music. Ameuza zaidi ya albamu milioni mbili na muziki wake umekuwa ukitumika kwenye filamu, televisheni, na michezo ya video. Mnamo mwaka 2009, alishinda tuzo ya Left Field Woodie inayotangazwa na mtvU.

Jina lake la kisanii lilitokana na bunduki ya nusu-otomatiki ya TEC-9, jina alilopewa na rapa Black Walt kutokana na mtindo wake wa kurap kwa kasi sana wa chopper. Yates baadaye alitoa maana ya ndani zaidi kwa jina hilo, akisema kuwa linasimama kwa mbinu kamili ya vina, ambapo "tech" inamaanisha mbinu (technique) na "nine" ikiwakilisha namba ya ukamilifu.

Maisha ya awali

Yates alizaliwa na kulelewa huko Kansas City, Missouri. Alianza kurap tangu akiwa mdogo sana, na alikuwa akirap herufi za jina lake ili kukumbuka jinsi ya kuliandika. Baba yake, Carlton Cook, hakuwa akiishi na familia na mama yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa na ugonjwa wa lupus tangu Yates akiwa mtoto, jambo ambalo lilimwathiri kihisia na kumfanya "amtafute Mungu". Alikuwa akitembelea majengo yaliyotelekezwa na rafiki yake mkubwa, akitumaini kupiga picha ya mzimu. Alisoma katika shule ya upili ya Southwest High School huko Kansas City.

Diskografia

Albamu za studio
  • The Calm Before the Storm (1999)
  • The Worst (2000)
  • Anghellic (2001)
  • Absolute Power (2002)
  • Everready (The Religion) (2006)
  • Killer (2008)
  • K.O.D. (2009)
  • All 6's and 7's (2011)
  • Something Else (2013)
  • Special Effects (2015)
  • The Storm (2016)
  • Planet (2018)
  • N9na (2019)
  • Enterfear (2020)
  • Asin9ne (2021)
  • Bliss (2023)
  • 5816 Forest (2025)
Mfululizo wa Collabos
  • Misery Loves Kompany (2007)
  • Sickology 101 (2009)
  • The Gates Mixed Plate (2010)
  • Welcome to Strangeland (2011)
  • Strangeulation (2014)
  • Strangeulation Vol. II (2015)
  • Dominion (2017)
  • Strange Reign (2017)
  • COSM (2024)

Filmografia

Makala za filamu (Documentaries)

Mwaka Jina
2003 Beef
2003 Das Bus
2004 T9X: The Tech N9ne Experience
2004 United Ghettos of America Vol. 2
2005 Hip Hop Nation Vol. 1
2005 Letter to the President
2008 The Psychumentary
2009 Strictly Strange
2010 K.O.D. Tour (Live in Kansas City)
2011 EuroTech Tour

Filamu

Mwaka Jina Uhusika
2009 The Life of Lucky Cucumber Yeye mwenyewe
2010 Big Money Rustlas Mhusika asiye na jina
2014 Vengeance Choco
2015 Night of the Living Dead: Origins 3D Zombie
2015 Alleluia! The Devil's Carnival The Librarian

Televisheni

Mwaka Jina Uhusika Maelezo
2009 Unsung Yeye mwenyewe Sehemu ya: "Zapp & Roger"
2012 Hip Hop Squares Yeye mwenyewe Sehemu 3
2013 When I Was 17 Yeye mwenyewe Sehemu ya: "Tech N9ne, Bam Margera, Olivia Munn"
2014 Wild 'n Out Yeye mwenyewe Sehemu ya 609

Read next

In 29 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article