Semaglutidi (Semaglutide), inayouzwa kwa majina ya chapa ya Ozempic miongoni mwa mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu Kisukari aina ya 2 na unene uliokithiri. Haipendekezwi sana kuliko metformin, ingawa zote mbili zinaweza kutumika pamoja. Dawa hii inaboresha udhibiti wa sukari ya damu, hupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo, na kupunguza hatari ya matatizo ya figo. Inatumika kwa kupitia mdomoni au kwa kudungwa sindano chini ya ngozi.
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuhara, maumivu ya tumbo, na kuvimbiwa choo. Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha ugonjwa wa kisukari wa asidi nyingi damuni, sukari ya chini ya damu, na kongosho. Kuna wasiwasi kwamba matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto, na kutumia wakati wa kunyonyesha hakupendekezwi. Dawa hii inafanya kazi kama glukagoni ya kibinadamu iliyo kama peptidi-1 (GLP-1) na huongeza kutolewa kwa insulini, inapunguza kutolewa kwa glukagoni, na kupunguza uondoaji wa votu tumboni.
Semaglutidi iliidhinishwa kwa matumizi ya matibabu nchini Marekani katika mwaka wa 2017. Iliundwa na shirika la Novo Nordisk na ilikuwa GLP-1 ya kwanza ambayo inaweza kuchukuliwa kupitia njia ya mdomo. Nchini Uingereza, miligramu mbili za sindano iligharimu Huduma ya Taifa ya Afya (NHS) takriban £73 kufikia mwaka wa 2020. Kiasi hiki nchini Marekani kiligharimu takriban Dola 850 kufikia mwaka wa 2021.