factograf
SW
Sign in

Ruth Jebet

Ruth Jebet

Key facts

tarehe ya kuzaliwa17 Novemba 1996
Urefu162cm
mahali alipozaliwaKenya

Ruth Jebet (alizaliwa tarehe 17 Novemba 1996) ni mwanariadha wa mbio ndefu na mtaalamu wa mita 3000 kuruka maji na vizuizi (steeplechase), mzaliwa wa Kenya anayewakilisha kimataifa taifa la Bahrain. Aliweka rekodi ya dunia katika matukio ya kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 na kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 2016 katika mbio za mita 3000 steeplechase. Mwezi desemba 2017, Ruth Jebet alisimamishwa kushiriki mashindano kwa miaka 4 (2018-2022) baada ya kupatikana na matumizi ya dawa ya EPO, inayotumika kuongeza uwezo wa kimichezo kinyume cha sheria za michezo.

Kazi

Jebet alichukua fursa ya kuwakilisha Bahrain akiwa na umri wa miaka kumi na sita, akifanya uhamisho wa ustahiki wake mnamo Februari 2013. Mnamo Aprili mwaka huo, alishinda mbio za mita 3000 na mita 5000 katika mashindano ya shule za upili nchini Kenya. Katika mashindano yake ya kwanza akiwania Bahrain, alishika nafasi ya pili katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi nyuma ya mwanariadha wa Olimpiki kutoka Moroko Salima El Ouali Alami katika Mashindano ya Riadha ya Kiarabu ya 2013. Muda wake wa dakika 9:52.47 uliweka rekodi ya kitaifa ya Bahrain katika tukio hilo. Aliongeza mafanikio yake mwezi Julai katika Mashindano ya Riadha ya Asia ya 2013, ambapo alichukua uongozi tangu mwanzo wa mbio na kuudumisha hadi mwisho. Alimshinda bingwa aliyetarajiwa kabla ya mbio na mshindi wa Michezo ya Asia Sudha Singh kwa zaidi ya sekunde kumi na tano. Muda wake wa dakika 9:40.84 uliweka rekodi ya ubingwa. Mafanikio haya yalimweka kama mmoja wa wakimbiaji bora wa mita 3000 kuruka viunzi barani Asia mwaka huo.

Mwaka 2014, akiwa na umri wa miaka 17, alishinda Mashindano ya Dunia ya Vijana mbele ya wanariadha wawili kutoka Kenya. Mwezi huo huo katika mashindano ya Weltklasse Zürich, aliweka rekodi ya bara la Asia kwa muda wa dakika 9:20.55, akikosa kwa sekunde 0.13 pekee kuvunja rekodi ya dunia ya vijana.

Katika Olimpiki ya Majira ya Joto ya 2016, alikua mwanariadha wa kwanza kutoka Bahrain kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki, baada ya kushinda mbio za mita 3000 kuruka viunzi kwa wanawake kwa muda wa 8:59.75, na kuwa mwanariadha wa pili kwa kasi zaidi katika historia ya tukio hilo wakati huo. Katika mbio hizo, alimshinda Mkenya Hyvin Jepkemoi, aliyeshinda medali ya fedha kwa muda wa 9:07.12, na Mmarekani Emma Coburn, aliyeshinda medali ya shaba kwa muda wa 9:07.63.

Marejeo

Makala hii kuhusu mwanariadha wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ruth Jebet kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Read next

In 30 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article