factograf
SW

Q

Alfabeti ya Kilatini
Aa Bb Cc Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz
(Kwa matumizi ya Kiswahili)
ch dh gh kh
mb mv nd ng ng' nj
ny nz sh th

Q ni herufi ya 17 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia alfabeti ya Kiswahili. Haitumiki katika mwandishi wa maneno ya Kiswahili isipokuwa kwa maneno ya kigeni.

Hapo sauti yake huwa ni "k". Hutokea mara nyingi pamoja na "u" kama "Qu" kwa sauti za "ku", "kw" au "kv". Hutumiwa pia kwa sauti ya ق (qaf) au "k ya shingoni" katika maneno ya Kiarabu kama vile "Qatar" yakiandikwa kwa alfabeti ya Kilatini.

Historia

Asili ya Q ni alama ya Qof katika mwandiko wa Kifinisia. Hakuna uhakika kuhusu maana asilia ya alama hiyo lakini herufi zote za Kifinisia zilitokana na picha zilizorahisishwa. Ilitumiwa kwa sauti ya "k ya shingoni" jinsi ilivyo hadi leo katika qaf ya Kiarabu.

Wagiriki wa Kale walipokea herufi za Wafinisia na kuziendeleza. Hawakuwa na sauti kama ile "qof" ya kifinisia. Awali waliita herufi hii Koppa na kuitumia kwa sauti ya "k" kabla ya "o" na "u" lakini baadaye hawakuona faida tena ya kuwa na alama mbili kwa "k" ileile wakafuta Koppa.

Alfabeti ya Kigiriki ilitumiwa na Waetruski huko Italia wakati Koppa bado ilikuwemo. Waliendelea kuitumia kwa sauti ya "ku" iliyotokea mara nyingi katikla lugha yao. Waroma wa Kale walipokea hivyo kutoka kwa Waetruski katika Kilatini. Mstari wa chini ukasogea kando jinsi ilivyo hadi leo.

In 149 languages

swAcèhAfrikaansAlemannischአማርኛaragonésÆngliscالعربيةܐܪܡܝܐasturianuazərbaycancaتۆرکجهBasa BaližemaitėškaBikol Centralбеларуская (тарашкевіца)беларускаяBetawiбългарскиবাংলাbòo pìkkàbrezhonegbosanskicatalà閩東語 / Mìng-dĕ̤ng-ngṳ̄کوردیcorsuqırımtatarcačeštinakaszëbscziчӑвашлаCymraegdanskDeutschZazakiΕλληνικάemiliàn e rumagnòlEnglishEsperantoespañoleestieuskaraفارسیsuomiNa Vosa VakavitiføroysktfrançaisNordfriiskfurlanFryskGaeilge贛語GàidhliggalegoAvañe'ẽBahasa HulontaloGaelgHausa客家語 / Hak-kâ-ngîעבריתहिन्दीhrvatskihornjoserbsceKreyòl ayisyenmagyarհայերենBahasa IndonesiaIgboIlokanoIdoíslenskaitaliano日本語ქართულიQaraqalpaqshaKumoring한국어کٲشُرkurdîкомиkernowekLatinaLëtzebuergeschLugandalombardlietuviųlatviešuMalagasyолык марийMinangkabauмакедонскиമലയാളംमराठीBahasa Melayuမြန်မာဘာသာمازِرونیNāhuatlNederlandsnorsk nynorsknorskNouormandNupeoccitanਪੰਜਾਬੀpolskiportuguêsRuna SimiromânăрусскийsicilianuScotsTaclḥitSimple EnglishslovenčinaslovenščinaanarâškielâchiShonaсрпски / srpskiSranantongoSeelterskSundasvenskaᥖᥭᥰ ᥖᥬᥲ ᥑᥨᥒᥰతెలుగుไทยTürkmençeTagalogSetswanatoki ponaTürkçeтатарча / tatarçaтыва дылукраїнськаاردوoʻzbekcha / ўзбекчаvènetovepsän kel’Tiếng ViệtVolapükwalonWinaray吴语хальмгმარგალურიייִדישYorùbá閩南語 / Bân-lâm-gí粵語中文

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article