factograf
SW

Njia ya Msalaba

Njia ya Msalaba
Kituo cha 12 – Yesu akifa msalabani. St. Raphael's Cathedral, Dubuque, Iowa, Marekani.
Kituo cha 12 – Yesu akifa msalabani. St. Raphael's Cathedral, Dubuque, Iowa, Marekani.
Njia ya msalaba ilivyopangwa katika kanisa kuu la Hong Kong, China.
Njia ya msalaba ilivyopangwa katika kanisa kuu la Hong Kong, China.
Station 5: Simoni wa Kirene akimsaidia Yesu kubeba msalaba, Maandamano ya Ijumaa Kuu 2011 huko Ulm, Ujerumani.
Station 5: Simoni wa Kirene akimsaidia Yesu kubeba msalaba, Maandamano ya Ijumaa Kuu 2011 huko Ulm, Ujerumani.
3 images

Njia ya Msalaba (kwa Kilatini, Via Crucis au Via Dolorosa) ni desturi ya sala inayolenga kumfuata Yesu Kristo hadi msalabani na kaburini.

Desturi hiyo ilianza Wakristo wa Ulaya walipozidi kutembelea Nchi takatifu katika Karne za Kati. Ni hasa wafuasi wa Fransisko wa Asizi walioeneza desturi hiyo kila mahali.

Mengi kati ya makanisa ya Wakatoliki yaani picha 14 zilizopangwa kwa kawaida ukutani kwa umbali fulani ili kuwezesha waamini kutembea kati ya moja na nyingine huku wakiendelea kutafakari juu ya mateso ya Yesu, jinsi ambavyo wangefanya mjini Yerusalemu, ili kuelewa zaidi upendo wa Mungu, kuchukia dhambi na kuzifidia.

Hata baadhi ya Walutheri na Waanglikana wanapenda desturi hiyo.

Desturi hiyo inaweza kufuatwa na mtu mmojammoja au kwa makundi hata makubwa.

Mbali ya kila Ijumaa ya mwaka, waamini wengi wanafuata njia hiyo wakati wa Kwaresima, na kwa namna ya pekee Ijumaa Kuu.

Mbali ya vituo 14 vilivyozoeleka zaidi, wengine wanapenda kuviongeza, kuvipunguza au kuvibadilisha hasa kwa kufuata zaidi habari za Injili na kumalizia na ufufuko wake.

Read next

In 51 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article