factograf
SW
Sign in

Mwigizaji wa Marekani

Michelle Rodriguez

Michelle Rodriguez

Key facts

tarehe ya kuzaliwa12 Julai 1978
kazimwigizaji
mahali alipozaliwaSan Antonio

Mayte Michelle Rodriguez alizaliwa 12 Julai 1978 anayejulikana kuigiza filamu kama Girlfight, The Fast and The Furious, Blue Crush, Resident Evil, S.W.A.T., na Avatar. Vilevile, ameigiza kama Ana Luzia Cortez kwenye kipindi cha Lost.

Maisha yake

Rodriguez alizaliwa mjini Bexar County, Texas. Yeye ni mtoto wa Carmen Milady na Rafael Rodriguez - aliyefanya kazi kwa jeshi la Marekani. Rodriguez alihamia nchini Dominican Republic alipokuwa na miaka minane pamoja na mamake na akaishi Puerto Rico mpaka alipofika miaka kumi na moja, na baadaye kuhamia mjini New Jersey. Rodriguez alijiunga na chuo kikuu na kusomea biashara lakini akaiacha na kujiunga na shule ya uigizaji, akiwa na azma ya kuwa mwandishi wa filamu.

Uigizaji

Rodriguez kwenye sherehe ya New York Fashion Week mnamo 2006
Rodriguez kwenye sherehe ya New York Fashion Week mnamo 2006
Filamu
Mwaka Filamu Aliigiza kama Maelezo
2000 Girlfight Diana Guzman
2001 The Fast and the Furious Letty
3 A.M. Salgado
2002 Blue Crush Eden
Resident Evil Rain Ocampo
2003 S.W.A.T. Chris Sanchez
2004 Control Teresa
2005 BloodRayne Katarin
2006 The Breed Nicki
2007 Battle in Seattle Lou
2008 A Cat's Tale Jujube Sauti
Gardens of the Night Lucy
2009 Fast & Furious Letty
Trópico de Sangre Minerva Mirabal
Avatar Trudy Chacon
2010 Machete Luz
2011 Battle: Los Angeles Corporal Adriana Santos
Army of Two Alice Murray
2012 Resident Evil: Retribution Rain Ocampo
Filamu
Mwaka Jina Aliigiza kama Vipindi
2005 Punk'd Mwenyewe 1
Immortal Grand Prix Liz Ricarro 26
2005-2006, 2009 Lost Ana Lucia Cortez 25
2007 Adventures in Voice Acting Mwenyewe 1

Mashtaka

Mnamo Machi 2002, Rodriguez alifungwa kwa ajili wa kumpiga rafiki yake. Madai haya yalitolewa pindi aliyempiga alipokataa kwenda kutoa ushahidi mahakamani. Mnamo Juni 2004, Rodriguez alishtakiwa kwa kuendesha gari ilhali alikuwa amelewa. Alipelekwa rumande kwa masaa 48.

Mnamo 2005, alipokuwa anarekodi Lost mjini Hawaii, alishikwa mara kadhaa na polisi kwa ajili ya kuvunja sheria barabarani na akatozwa faini ya $357.

Maisha ya kibinafsi

Mnamo 2000, alipendana na Muislamu lakini akaachana naye akisema kuwa dini hiyo ina sheria nyingi. Mnamo 2003, Rodriguez ameonekana akiwa na muigizaji Olivier Martinez nchini Ufaransa.

Read next

In 76 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article