factograf
SW
Sign in

Mathieu Kassovitz

Mathieu Kassovitz

Key facts

tarehe ya kuzaliwa3 Agosti 1967
kazimwigizaji, Mtayarishaji wa filamu, mwongozaji wa filamu
mwenziJulie Mauduech

Mathieu Kassovitz (alizaliwa 3 Agosti 1967) ni mwigizaji, mkurugenzi wa filamu, mtayarishaji wa filamu na mwandishi wa miswada ya filamu kutoka Ufaransa. Amewahi kushinda tuzo tatu za César: tuzo ya Mwigizaji Chipukizi Anayeahidi Zaidi kupitia filamu See How They Fall (1994), pamoja na tuzo za Filamu Bora na Uhariri Bora kupitia filamu La Haine (1995). Pia aliwahi kuteuliwa kuwania tuzo za Mkurugenzi Bora na Mwandishi Bora wa Muswada Asilia au Urekebishaji.

Maisha ya awali

Mathieu Kassovitz ni mtoto wa Peter Kassovitz, mtayarishaji, mkurugenzi na mwandishi wa filamu, na Chantal Rémy, mhariri wa filamu.

Mama yake ni Mfaransa na Mkatoliki, huku baba yake akiwa Myahudi mwenye asili ya Hungaria ambaye alikimbia nchini humo wakati wa Mapinduzi ya Hungaria ya mwaka 1956.

Mathieu amewahi kujieleza kwa kusema: “Mimi si Myahudi, lakini nililelewa katika mazingira ya ucheshi wa Kiyahudi.”

Marejeo

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mathieu Kassovitz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Read next

In 48 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article