factograf
SW

Maajabu ya dunia

Maajabu ya dunia

Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa Kale. Wagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).

Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon

Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika ustaarabu huo. Kwa hiyo hakuna mifano kutoka Uhindi, China, Asia ya Mashariki, Amerika, Afrika kusini ya Sahara wala Ulaya ya Kaskazini.

Majengo ya orodha ya Antipater hayakudumu hadi leo, isipokuwa Piramidi za Giza. Mengine yaliharibika kutokana na matetemeko ya ardhi au kubomolewa, tena hadi leo hapajulikani mahali pa "Mabustani ya Semiramis". Sanamu na picha za kuchongwa kutoka Kaburi la Mausolo na Hekalu la Artemis zilikusanwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Britania mjini London, Uingereza.

Maajabu saba ya Kale

Maajabu ya dunia ya sasa

Katika ulimwengu kila siku maajabu yanaongezeka na kufanya maajabu mapya ya dunia kukubalika mara kwa mara. Kwa mfano, mwaka 2016 kuna maajabu yake. Orodha ya maajabu hayo hutolewa na watu mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti: wengine wanaishia upande wa majengo, wengine wanahesabu hata mazuri ya uasilia n.k.

Vitu hivi hadi kufikia kuitwa maajabu ya dunia ina maana ni vya pekee duniani kote, na hakuna kitu kingine kama hicho au cha kufanana nacho.

Tanzania kuna kitu kimoja ambacho kinasemekana ni kati ya maajabu ya dunia ambacho ni kasoko ya Ngorongoro, iliyoko mkoa wa Manyara.

Picha za "Maajabu ya Kisasa"

Hagia Sophia, Istanbul, Uturuki
Hagia Sophia, Istanbul, Uturuki
Mawe yaliyobebana huko Stonehenge, Uingereza
Mawe yaliyobebana huko Stonehenge, Uingereza
Machu Picchu, Peru
Machu Picchu, Peru
Taj Mahal, India
Taj Mahal, India
Ghorofa za New York, Marekani
Ghorofa za New York, Marekani
Daraja la geti la shaba
Daraja la geti la shaba
Maporomoko ya Viktoria, Zambia-Zimbabwe
Maporomoko ya Viktoria, Zambia-Zimbabwe
Miamba tumbawe ya Great Barrier Reef, Australia
Miamba tumbawe ya Great Barrier Reef, Australia
Mnara wa ON, Toronto, Kanada
Mnara wa ON, Toronto, Kanada
9 images

Marejeo

  • D'Epiro, Peter, and Mary Desmond Pinkowish, "What Are the Seven Wonders of the World? and 100 Other Great Cultural Lists". Anchor. 1 December 1998. ISBN 0-385-49062-3
  • "The Seven Wonders of the World, a History of Modern Imagination" written by John & Elizabeth Romer in 1995
  • "The Seven Wonders of the Ancient World" edited by Peter Clayton and Martin Price in 1988
  • Johann Conrad Orelli (ed.) Philonis Byzantini Libellus de septem orbis spectaculis. 1816. The original travel guide by Pseudo-Philo
  • Lendering, Jona (2007–2010). "Seven Wonders of the Ancient World". Livius.Org. Iliwekwa mnamo 28 Julai 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

  • "Seven Ancient Wonders of the World" on The History Channel website. Also includes links to medieval, modern and natural wonders.
  • Parkin, Tim, Researching Ancient Wonders: A Research Guide, from the University of Canterbury, New Zealand. – a collection of books and Internet resources with information on seven ancient wonders.
  • "Eternal wonder of humanity's first great achievements", by Jonathan Glancey in The Guardian, 10 March 2007
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maajabu ya dunia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Read next

In 113 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article