Kongwa (kwa Kiingereza: yoke) ni fimbo yenye panda au mgawanyiko ambayo zamani ilitumika kwa kuwafunga wanyama ili kuvuta ama mkokoteni ama plau au watumwa shingoni ili kuwasafirisha.
Wakati wa biashara ya watumwa, makongwa yalikatwa mtini. Wafungwa walioonyesha nia na uwezo wa kutoroka walifungiwa kongwa shingoni. Mara nyingi makongwa mawili yalifungwa pamoja, hali iliyooongeza ugumu wa kukimbia.
Katika Biblia
Mfano wa kongwa ulitumika sana katika Agano la Kale na katika Agano Jipya kwa namna mbalimbali, kama vile kuhusu unyanyasaji katika jamii (1Fal 12:4) na kuhusu dhambi iliyofunga na kulemea watu (Mao 1:14).
Torati pia ilifananishwa na kongwa ambayo ilifanywa nzito zaidi na mafundisho ya Mafarisayo hata kulemea waumini (Mdo 15:10). Ndiyo maana Yesu aliwaalika kuachana nao ili kupokea kongwa lake (Math 11:28-30).
Hatimaye Mtume Paulo aliita kongwa la utumwa (Gal 5:1) ambalo Yesu ametuondolea ili tuwe huru, hivyo tusikubali kutekwa tena.
