James Christopher Armfield (21 Septemba 1935 – 22 Januari 2018) alikuwa mchezaji na kocha wa mpira wa miguu kutoka nchini Uingereza. Alicheza katika Ligi ya Uingereza katika klabu ya Blackpool, mara nyingi akicheza nafasi ya beki wa kulia. Kati ya mwaka 1954 na 1971, alicheza mechi 627 katika mashindano yote, akafunga mabao sita, na alihudumu kama nahodha wa klabu hiyo kwa muongo mmoja. Pia aliitumikia timu ya taifa ya Uingereza mara 43 kati ya mwaka 1959 na 1966, na alikuwa nahodha wao katika mechi 15. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Uingereza kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA mwaka 1966. Baada ya kustaafu kucheza mpira, Armfield alizifundisha klabu za Bolton Wanderers na Leeds United, akiivusha Leeds United hadi fainali ya mashindano ya ulaya mwaka 1975.
Marejeo
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jimmy Armfield kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
