factograf
SW

Bwawa la Malebo

Bwawa la Malebo

Key facts

ni mfano waziwa
NchiJamhuri ya Kongo
ipo katika eneo la kiutawalaKinshasa
Bwawa la Malebo linavyoonekana kwa macho ya ndege kutoka upande wa Kinshasa
Bwawa la Malebo linavyoonekana kwa macho ya ndege kutoka upande wa Kinshasa

Bwawa la Malebo (far. Pool Malebo, majina mengine Malebo Pool, zamani Stanley Pool, pia Ziwa Ngobila au Ziwa Nkunda) ni sehemu ya mwendo wa mto Kongo ambako mto unapanuka sana kwa urefu wa kilomita 35 ukifikia upana wa kilomita 23.


Jina

Jina la Malebo latokana na jina la kienyeji "lilebo (uwingi malebo)" kwa miti ya aina mchapa (Borassus flabellifer) inayopatikana kwa wingi hapo.

Jina la zamani Stanley Pool latokana na Henry Morton Stanley aliyefika hapa mwaka 1877 akaanzisha kituo cha Léopoldville, kitangulizi cha mji wa Kinshasa.

Jiografia

Miji mikuu ya Kinshasa na Brazzaville iko kando la bwawa hili ikitazamana.

Sehemu ya mto Kongo inayopitika kwa meli ndogo za mtoni kwenda hadi Mbandaka, Kisangani na Bangui inaanza hapa. Chini ya bwawa kuna maporomoko ya Livingstone yanayozuia usafiri kwa maji hadi bahari.

Viungo vya Nje

  • Joint Operations Graphic (Air) 1:250,000, Ramani SB-33-3

Read next

In 43 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article