
Belzebuli (kwa Kiingereza: Beelzebul au Beelzebub, kutoka Kiebrania בַּעַל־זְבוּב, Baʿal-zəḇūḇ, yaani Bwana wa nzi) ni umbo la dharau la jina Baʿal zəvul, yaani Bwana wa mbingu, mungu mmojawapo kati ya ile iliyoabudiwa katika Mashariki ya Kati ya kale, hasa na Wafilisti wa Ekron, ambalo tena linahusiana na Baali, mungu mkuu wa Kanaani.
Umbo hilo lilitumika katika Agano Jipya kama jina lingine la shetani) likazidi kutumiwa na Wayahudi, Wakristo na Waislamu kama jina la mmojawapo kati ya pepo wakuu zaidi.
Kwa Kiarabu jina limekuwa Baʿlzabūl (بعلزبول).
Viungo vya nje
- Catholic Encyclopedia: Beelzebub
- Jewish Encyclopedia: Beelzebub
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
