factograf
SW

unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi

Ajira kwa watoto

Ajira kwa watoto
Mtoto wa Kichina akitengeneza viatu, mwishoni mwa karne ya 19
Mtoto wa Kichina akitengeneza viatu, mwishoni mwa karne ya 19

Ajira kwa watoto inarejelea unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo inawanyima utoto wao, inaingilia uwezo wao wa kuhudhuria shule ya kawaida, na inawadhuru kiakili, kimwili, kijamii na kimaadili. Unyonyaji kama huo umepigwa marufuku na sheria duniani kote, ingawa sheria hizo hazihesabu kazi zote za watoto kama ajira yao; kwa mfano kazi za usanii, majukumu ya familia, mafunzo yanayosimamiwa, na baadhi ya aina za kazi za watoto zinazofanywa kimalezi. Umaskini na ukosefu wa shule vinachukuliwa kuwa sababu kuu ya ajira kwa watoto.

Historia

Ajira kwa watoto imekuwepo kwa viwango tofauti katika historia. Wakati wa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, watoto wengi wenye umri wa miaka 5-14 kutoka familia maskini walifanya kazi katika mataifa ya Magharibi na makoloni yao. Watoto hao walifanya hasa kazi za kilimo, viwandani, uchimbaji madini na wengine walifanya kazi za usiku za masaa 12. Kwa kuongezeka kwa mapato ya kaya, upatikanaji wa shule na kupitishwa kwa sheria za ajira kwa watoto, viwango vya matukio ya ajira ya watoto vilipungua.

Katika nchi maskini zaidi duniani, karibu mtoto mmoja kati ya wanne wana ajira, idadi kubwa kati yao (asilimia 29) wanaishi nchi za Afrika kusini kwa Jangwa la Sahara. Mnamo mwaka 2017, mataifa manne za Afrika (Mali, Benin, Chad na Guinea Bisau) walishuhudia zaidi ya asilimia 50 ya watoto wenye umri wa miaka 5-14 wakifanya kazi. Kilimo duniani kote ndicho mwajiri mkubwa zaidi wa watoto. Idadi kubwa ya ajira hizo hupatikana vijijini na katika uchumi usio rasmi wa mijini; watoto huajiriwa zaidi na wazazi wao, badala ya viwanda.

Matukio ya ajira kwa watoto yalipungua ulimwenguni kutoka 25% hadi 10% kati ya mwaka 1960 na 2003, kulingana na Benki ya Dunia. Hata hivyo, jumla ya idadi ya watoto wanaotumikishwa bado ni kubwa, huku shirika la Mfuko wa Kimataifa wa Watoto (UNICEF) na Shirika la kimataifa la kazi (ILO) zikikubali wastani wa watoto milioni 168 wenye umri wa miaka 5-17 duniani kote walihusika katika ajira kwa watoto mwaka 2013.

Picha

Watoto wakifanya kazi, Macon, Georgia, 1909
Watoto wakifanya kazi, Macon, Georgia, 1909
Watoto wanaofanya kazi katika shughuli za mikusanyiko ya nyumbani nchini Marekani (1923).
Watoto wanaofanya kazi katika shughuli za mikusanyiko ya nyumbani nchini Marekani (1923).
Wasichana wawili wakipinga ajira ya watoto (kwa kuuita utumwa wa watoto) jijini New York City 1909 katika gwaride la siku ya wafanyakazi.
Wasichana wawili wakipinga ajira ya watoto (kwa kuuita utumwa wa watoto) jijini New York City 1909 katika gwaride la siku ya wafanyakazi.
Arthur Rothstein, Ajira ya watoto, Cranberry Bog, 1939. Brooklyn Museum
Arthur Rothstein, Ajira ya watoto, Cranberry Bog, 1939. Brooklyn Museum
4 images

Read next

In 69 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article