factograf
SW

Run-D.M.C.

Run-D.M.C.

Key facts

kuanzishwa1981
ni mfano wakundi la muziki
ainaEast Coast hip hop
All data from the card 6
Asili yake
Queens, New York, US
Aina ya muziki
Muziki wa hip hop, rap rock
Miaka ya kazi
1983 - 2002
Studio
Profile, Def Jam
Ame/Wameshirikiana na
Beastie BoysLL Cool JAerosmithPublic EnemySlick RickJason NevinsKid RockOnyx
Tovuti
www.RunDMC.com


Run-DMC (pia huandikwa kama Run-D.M.C., RUN DMC, au mchanganyiko wowote wa majina hayo ni sawa tu) lilikuwa kundi la muziki wa hip hop kutka nchini Marekani. Kundi lilianzishwa mwaka wa 1983 katika mtaa wa Hollis, Queens, New York City na Joseph Simmons, Darryl McDaniels, na Jason Mizell. Run-DMC linachukuliwa kama moja ya vikundi vyenye ushawishi mkubwa katika historia ya tamaduni ya hip hop na hasa huwekwa katika zama za kizazi cha dhahabu cha hip hop katika miaka ya 1980. Pamoja na Beastie Boys, LL Cool J, DJ Jazzy Jeff & the Fresh Prince, na Public Enemy. Kundi hili lilikuwa miongoni mwa waasisi wa muziki wa hip hop wa shule mpya na kusaidia kuanzisha enzi ya dhahabu ya hip hop. Kundi hili lilikuwa miongoni mwa ya kwanza kuonyesha umuhimu wa uhusiano kati ya MC na DJ.

Kwa kutolewa kwa albumu ya Run-D.M.C. (1984), Run-DMC lilikuwa kundi la kwanza la hip hop kupata rekodi ya Dhahabu. Albumu ya Run-D.M.C. ilifuatwa na King of Rock (1985), ambayo ilithibitishwa kama Platinum, ikifanya Run-DMC kuwa kundi la kwanza la hip hop kufikia Platinum. Raising Hell (1986) ilikuwa rekodi ya kwanza ya hip hop kuwa na mauzo ya multi-platinum. Miondoko ya Run-DMC ya wimbo wa "Walk This Way", ikiwa na ushirikiano wa kundi la Aerosmith, iliweza kufikia nafasi ya juu zaidi kwenye orodha ya Billboard Hot 100 kuliko toleo la awali la Aerosmith, ikifika nambari nne. Wimbo huu ulijulikana sana katika muziki wa hip hop na rock. Run-DMC lilikuwa kundi la kwanza la hip hop kuonesha video zao za muziki kwenye MTV, kuonekana kwenye American Bandstand, kuwa kwenye jalada la Rolling Stone, kutumbuiza kwenye Live Aid, na kupokea tuzo ya Grammy.

Mnamo mwaka wa 2004, Rolling Stone lilikiweka Run-DMC katika nafasi ya 48 kwenye orodha yake ya Wasanii 100 Bora wa Wakati Wote. Mwaka 2007, walitunukiwa tuzo ya The Greatest Hip Hop Group of All Time na MTV na Greatest Hip Hop Artist of All Time na VH1. Mwaka 2009, Run-DMC lilikuwa kundi la pili la hip hop (baada ya Grandmaster Flash & the Furious Five, 2007) kuingizwa katika Rock and Roll Hall of Fame. Mwaka 2016, kundi hili lilipokea Tuzo ya Grammy Lifetime Achievement Award. Mnamo mwaka wa 2018, albumu ya Raising Hell ilingizwa katika National Recording Registry na Library of Congress kwa kuwa na umuhimu wa "kitamaduni, kihistoria, au kimaumbile."

Diskografia

Albamu

Mwaka Albamu Chati
Billboard 200 US Hip-Hop RIAA
1984 Run-D.M.C. 53 14 Gold
1985 King of Rock 52 12 Platinum
1986 Raising Hell 3 1 3x Platinum
1988 Tougher Than Leather 9 2 Platinum
1990 Back from Hell 81 16 300,000
1993 Down with the King 7 1 Gold
2001 Crown Royal 37 22 Gold

Singles

Year Title U.S. Hot 100 U.S. R&B Album
1983 "It's like That" - 15 Run-D.M.C.
1984 "30 Days" - 16
"Hard Times" - 11
"Hollis Crew (Krush Groove 2)" - 65
1985 "Can You Rock It Like This" - 19 King of Rock
"Jam-Master Jammin'" - 53
"King of Rock" - 14
"You Talk Too Much" - 19
1986 "My Adidas" - 5 Raising Hell
"Walk This Way" 4 8
"You Be Illin'" 29 12
1987 "It's Tricky" 57 21
1988 "I'm Not Going Out Like That" - 40 Tougher Than Leather
"Mary, Mary" 75 29
"Run's House" - 10
1989 "Pause" - 51 Back From Hell
1990 "What's It All About" - 24
1991 "Faces" - 57
1993 "Down with the King" 21 9 Down with the King
"Ooh, Whatcha Gonna Do" - 78
2001 "Rock Show" - - Crown Royal

Greatest hits albamu

  • Together Forever: Greatest Hits 1983–1991 (1991) (Profile Records)
  • High Profile: The Original Rhymes (2002) (Profile Records)
  • Greatest Hits (2002) (Profile Records)
  • The Best of Run-D.M.C. (2003) (Profile Records)
  • Ultimate Run-D.M.C. (2003) (Profile Records)
  • Artist Collection: Run-D.M.C. (2004) (Arista Records)
  • Live At Montreux 2001 (2007) (Eagle Records)

In 39 languages

Text from Wikipedia, CC BY-SA 4.0 · Source article